All posts by Mary Kigosi

WANAWAKE CHUO KIKUU ARDHI WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

WANAWAKE CHUO KIKUU ARDHI WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Wanawake wa Chuo Kikuu Ardhi wameshiriki kwenye sherehe za kuadhimisha siku ya wanawake duniani zilizofanyika Mwembe yanga wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam.

Maadhimisho hayo ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 08/03 yamezinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke mhe. Felix Lyaviva ambapo alisisitiza wanawake kujituma Zaidi ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Mbali na Chuo Kikuu Ardhi, maadhimisho hayo pia yalihudhuriwa na wanawake kutoka maeneo mbalimbali yakiwemo Wizara, mashirika na taasisi mbalimbali za umma na binafsi.

MATUKIO MBALIMBALI YA PICHA

DSC_0094Baadhi ya wanawake wa Chuo Kikuu Ardhi wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maandamano ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Temeke mwembe yanga. Continue reading WANAWAKE CHUO KIKUU ARDHI WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AHITIMISHA ZIARA ZA MIRADI MBALIMBALI KATIKA VIWANJA VYA CHUO KIKUU ARDHI

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AHITIMISHA ZIARA ZA MIRADI MBALIMBALI KATIKA VIWANJA VYA CHUO KIKUU ARDHI

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi jana alihitimisha ziara za kutembelea miradi mbalimbali inayofanywa na wilaya yake jana kwa kufanya mkutano katika viwanja vya Chuo Kikuu Ardhi, ambapo kabla ya kuanza mkutano Mhe. Hapi alifika ofisini kwa Makamu Mkuu wa Chuo kusaini kitabu cha wageni baadaye aliambatana na viongozi wa chuo kwaajili ya mkutano.

Mkutano huo ulikuwa kwaajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wake na kuruhusu maswali juu ya kero hizo. Aidha Mhe. Hapi aliambatana na wakuu wa idara mbalimbali wa wilaya ili kuweza kujibu kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Mhe. Hapi alimaliza kwa kuwashukuru wenyeji wake Chuo Kikuu Ardhi kwa kuwapatia uwanja wa kufanyia mkutano wa kuhitimisha ziara zake za kutembelea miradi mbalimbali katika wilaya yake.  

IMG-20170303-WA0008Mhe. Ally Hapi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni akiwa na viongozi wa Chuo Kikuu Ardhi kushoto ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Gabriel Kassenga, kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Mipango, Fedha na Utawala Prof. Evaristo Liwa. Continue reading MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AHITIMISHA ZIARA ZA MIRADI MBALIMBALI KATIKA VIWANJA VYA CHUO KIKUU ARDHI

Chuo Kikuu Ardhi chaeleza ushiriki wake katika masuala mbalimbali ya maendeleo ya uchumi na jamii nchini

Chuo Kikuu Ardhi chaeleza ushiriki wake katika masuala mbalimbali ya maendeleo ya uchumi na jamii nchini

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Idrissa Mshoro ameelezea ushiriki wa chuo chake katika baadhi ya masuala muhimu ya nchi na kutokana na taaluma zinazofundishwa na kufanyiwa tafiti na chuo chake.

Ameeleza hayo jana alipokuwa na mkutano na waandishi na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa habari maelezo, alisema utafiti huu unahusisha ujenzi wa kuta za jingo kwa kumimina mchanganyiko mahsusi wa saruji, mchanga na kemikali maalum kwa kutumia kingo za plastiki (plastic formwork) zinazoweza kutumika hadi mara hamsini baada ya matumizi ya awali. Continue reading Chuo Kikuu Ardhi chaeleza ushiriki wake katika masuala mbalimbali ya maendeleo ya uchumi na jamii nchini

TUSIIME FORM SIX STUDENTS WHO TAKING GEOGRAPHY SUBJECT VISIT ARDHI UNIVERSITY SCHOOL OF EARTH SCIENCES, REAL ESTATES, BUSINESS AND INFORMATICS (SERBI)

TUSIIME FORM SIX STUDENTS WHO TAKING GEOGRAPHY SUBJECT VISIT ARDHI UNIVERSITY SCHOOL OF EARTH SCIENCES, REAL ESTATES, BUSINESS AND INFORMATICS (SERBI)

 DSC_0758Form six students from Tusiime Secondary School taking some notes from ARU expert during the visitation. Continue reading TUSIIME FORM SIX STUDENTS WHO TAKING GEOGRAPHY SUBJECT VISIT ARDHI UNIVERSITY SCHOOL OF EARTH SCIENCES, REAL ESTATES, BUSINESS AND INFORMATICS (SERBI)

MAFUNZO JUU YA UWELEWA WA DHANA YA MAAFA, UHUSIANO WAKE NA MAENDELEO NA JITIHADA ZA KUPUNGUZA MAAFA KATIKA JAMII.

MAFUNZO JUU YA UWELEWA WA DHANA YA MAAFA, UHUSIANO WAKE NA MAENDELEO NA JITIHADA ZA KUPUNGUZA MAAFA KATIKA JAMII.

JIJINI MWANZA:

Tarehe: 10.2.2017

Kituo cha mafunzo ya menejimenti ya Maafa Chuo Kikuu Ardhi (DMTC) kiliendesha mafunzo ya siku moja jijini Mwanza.Mafunzo hayo yalilenga watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza na watendaji wa kata zote za Jiji juu ya uelewa wa dhana ya maafa na uhusiano wake na maendeleo na jitihada za kupunguza maafa katika jamii.

20170210_094603Mkufunzi wa kitengo hicho Dkt.F.Mgendi akitoa mada ya dhana ya maafa katika mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza wilaya ya Ilemela,na kulia kwake aliyeketi ni Mkuu wa Kitengo hicho Prof. R. Kiunsi akisikiliza wakati mafunzo yakiendelea.

20170210_095814Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali ziliwasilishwa wakati wa mafunzo.

UONGOZI WA CHUO KIKUU ARDHI LEO UMEWAAGA WANAMICHEZO WANAFUNZI WATAKAOSHIRIKI MASHINDANO YA MICHEZO YA AFRIKA MASHARIKI YA VYUO VIKUU VYOTE YATAKAYOFANYIKA NCHINI KENYA.

UONGOZI WA CHUO KIKUU ARDHI LEO UMEWAAGA WANAMICHEZO WANAFUNZI WATAKAOSHIRIKI MASHINDANO YA MICHEZO YA AFRIKA MASHARIKI YA VYUO VIKUU VYOTE YATAKAYOFANYIKA NCHINI KENYA KUANZIA TAREHE 16/12/2016

????????????????????????????????????

Makamu Mkuu wa Chuo Prof.  Idrissa Mshoro akitoa neno fupi kwa wanafunzi wanamichezo wa Chuo Kikuu Ardhi katika ukumbi Council ambao wanakwenda kuipeperusha bendera ya Chuo katika mashindano ya michezo ya vyuo vikuu vya Afrika Mashariki yatakayofanyika nchini Kenya. Continue reading UONGOZI WA CHUO KIKUU ARDHI LEO UMEWAAGA WANAMICHEZO WANAFUNZI WATAKAOSHIRIKI MASHINDANO YA MICHEZO YA AFRIKA MASHARIKI YA VYUO VIKUU VYOTE YATAKAYOFANYIKA NCHINI KENYA.

KONGAMANO NA MKUTANO WA TANO WA BARAZA LA WAHITIMU LA CHUO KIKUU ARDHI LILILOFANYIKA TAREHE 02/12/2016 ARCH PLAZA

KONGAMANO NA MKUTANO WA TANO WA BARAZA LA WAHITIMU LA CHUO KIKUU ARDHI LILILOFANYIKA TAREHE 02/12/2016 ARCH PLAZA

Chuo Kikuu Ardhi kimekuwa na utaratibu wa kila mwaka kuandaa Kongamano na Mkutano wa Baraza la Wahitimu ambapo kwa mwaka huu ni Kongamano la nne na Mkutano wa tano uliokuwa unajadili mada inayohusu “ardhi, haki za ardhi, usawa pamoja na maendeleo yake ambapo majadiliano hayo yanalenga kuwajengea uelewa wahitimu hao katika kukuza na kuboresha sekta nzima ya ardhi na ujenzi kwa ajili ya kukuza maendeleo ya nchi nzima,”

 Mgeni rasmi katika kongamano hilo alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Moses Kusiluka ambaye alizungumzia “ukuaji wa nchi na maendeleo yake huchangiwa na mipango bora ya matumizi ya ardhi unaotekelezwa na wananchi hasa wale wanaohusika katika shughuli za ujenzi wa miundombinu.”

Aidha Dkt. Kusiluka amekipongeza Chuo Kikuu Ardhi  kwa kushirikiana na Serikali pamoja na jamii katika kuboresha sekta ya ardhi pamoja na sekta ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali kwa kutoa elimu bora kwa wanafunzi ambao watakuja kuwa wataalam wazuri kwa siku zijazo.

_DSC0928Mgeni rasmi katikati mbele Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Moses Kusiluka akiwasili Arch Plaza tayari kwa kufungua Kongamano la Wahitimu la Chuo Kikuu Ardhi. Continue reading KONGAMANO NA MKUTANO WA TANO WA BARAZA LA WAHITIMU LA CHUO KIKUU ARDHI LILILOFANYIKA TAREHE 02/12/2016 ARCH PLAZA

SHEREHE YA KUWATUNUKU WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI KITAALUMA

SHEREHE YA KUWATUNUKU WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI KITAALUMA

Chuo Kikuu Ardhi kimekuwa na utaratibu wa kila mwaka kufanya sherehe za kuwatunuku wanafunzi zawadi na tuzo mbalimbali siku moja kabla ya mahafali ya Chuo, ambapo jumla ya wanafunzi 104 walitunukiwa zawadi na tuzo mbalimbali. Katika sherehe hizo jumla ya wanafunzi wanne kati ya waliofanya vizuri wamepata alama sawa hivyo kuibuka washindi wa jumla kwa mwaka 2016.

MATUKIO YA PICHA WAKATI WA SHEREHE ZA KUWATUNUKU ZAWADI NA TUZO MBALIMBALI SIKU YA IJUMAA TAREHE 02/12/2016

_DSC0792Mmoja kati ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi akipokea Cheti kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Idrissa B. Mshoro wakati  sherehe za kuwatuku zawadi mbalimbali wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao. Continue reading SHEREHE YA KUWATUNUKU WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI KITAALUMA