ARU ORGANIZES INDUCTION COURSE FOR THE NEWLY APPOINTED LEADERS

ARU ORGANIZES INDUCTION COURSE FOR THE NEWLY APPOINTED LEADERS

The management of ARU has organized induction course for the new leaders so as to equip them with additional knowledge towards leading their units and directorate.

The training which was facilitated by different conversant people in human resources management was held at APC Mbweni on 3rd and 4th of May 2017. About 45 ARU leaders namely Deans, Directors and Heads from different units participated.

7Some of the  participants on leadership induction course. Continue reading ARU ORGANIZES INDUCTION COURSE FOR THE NEWLY APPOINTED LEADERS

CHUO KIKUU ARDHI WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI TAREHE 01/05/2017

CHUO KIKUU ARDHI WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI TAREHE 01/05/2017

Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi waungana na wafanyakazi wote duniani kuadhimisha siku ya wafanyakazi ambayo kitaifa imefanyika mkoani Kilimanjaro mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Chuo Kikuu Ardhi waliungana na wafanyakazi kutoka mashirika na taasisi mbalimbali mkoani Dar es Salaam kuadhimisha siku ya wafanyakazi katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

20170501_092227Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi wakiingia uwanja wa Uhuru wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani.

Continue reading CHUO KIKUU ARDHI WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI TAREHE 01/05/2017

CHUO KIKUU ARDHI CHATEKELEZA AGIZO LA SERIKALI LA KUFANYA MAZOEZI YA VIUNGO KILA JUMAMOSI YA PILI YA MWEZI

CHUO KIKUU ARDHI CHATEKELEZA AGIZO LA SERIKALI LA KUFANYA MAZOEZI KILA JUMAMOSI YA PILI YA MWEZI

Katika kutekeleza agizo la serikali la kuwataka wananchi kufanya mazoezi ya viungo kila Jumamosi ya pili ya mwezi, uongozi wa Chuo Kikuu Ardhi ikishirikiana na Idara ya michezo iliandaa mazoezi ya viungo yaliyofanyika katika viwanja vya ARU ambapo yalitanguliwa na matembezi ya umbali wa kilomita tatu (3) yalioanzia jengo la Utawala la Chuo Kikuu Ardhi kuzunguka maeneo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mazoezi hayo yaliongozwa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Gabriel Kassenga sambamba na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo -Mipango, Fedha na Utawala Prof. Evaristo Liwa.

20170408_071825Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Gabriel Kassenga (katikati) kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo -Mipango, Fedha na Utawala Prof. Evaristo Liwa, kushoto ni Mkufunzi wa Michezo Bw. Boniface Tamba. Continue reading CHUO KIKUU ARDHI CHATEKELEZA AGIZO LA SERIKALI LA KUFANYA MAZOEZI YA VIUNGO KILA JUMAMOSI YA PILI YA MWEZI

MRADI WA UJENZI WA TEKNOLOJIA YA GHARAMA NAFUU UNAOSIMAMIWA NA CHUO KIKUU ARDHI – MAHAKAMA YA KINYEREZI JIJINI DAR ES SALAAM

MRADI WA UJENZI WA TEKNOLOJIA YA GHARAMA NAFUU UNAOSIMAMIWA NA CHUO KIKUU ARDHI – MAHAKAMA YA KINYEREZI JIJINI DAR ES SALAAM

DSC_0335Jengo la mahakama ya kinyerezi ambalo linalokaribia kukamilika kwa ujenzi huo wa gharama nafuu. Continue reading MRADI WA UJENZI WA TEKNOLOJIA YA GHARAMA NAFUU UNAOSIMAMIWA NA CHUO KIKUU ARDHI – MAHAKAMA YA KINYEREZI JIJINI DAR ES SALAAM

KUFUNGWA KWA MTAMBO YA SATELLITE CHUO KIKUU ARDHI

KUFUNGWA KWA MTAMBO WA SATELLITE CHUO KIKUU ARDHI

Skuli ya Sayansi dunia, Uwekezaji katika miliki, Biashara na Infomatikia (SERBI) kwa udhamini wa   MESA (Monitoring for Environment and Security in Africa) wamefunga mtambo kwa ajili ya kunasa data za satellite (MODIS) na pia kutoa taarifa za majanga mbalimbali Kama Moto, mafuriko na ukame Kwa wakati nchini na maeneo ya SADC Kwa ujumla.

Katika kufanikisha hilo MESA walileta wataalaumu wawili ambao ni Bi. Masebo Rachel Nkepu kutoka Botswana na Bw. Mkise Steve Masha kutoka Afrika Kusini ili kuweza kutoa mafunzo mafupi kwa baadhi ya wataalamu kutoka Skuli ya Sayansi dunia, Uwekezaji katika Miliki, Biashara na Infomatikia juu ya uwezeshaji na ufuatiliaji wa mtambo huo ili kuweza kutunza kumbukumbu za majanga mbalimbali yanayoweza kutokea.

DSC_0064Bi. Masebo Rechal Nkepu kutoka Botswana akiweka lebo ya MESA mara baada ya kufungwa mtambo wa Satellite Chuo Kikuu Ardhi. Continue reading KUFUNGWA KWA MTAMBO YA SATELLITE CHUO KIKUU ARDHI

WANAWAKE CHUO KIKUU ARDHI WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

WANAWAKE CHUO KIKUU ARDHI WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Wanawake wa Chuo Kikuu Ardhi wameshiriki kwenye sherehe za kuadhimisha siku ya wanawake duniani zilizofanyika Mwembe yanga wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam.

Maadhimisho hayo ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 08/03 yamezinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke mhe. Felix Lyaviva ambapo alisisitiza wanawake kujituma Zaidi ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Mbali na Chuo Kikuu Ardhi, maadhimisho hayo pia yalihudhuriwa na wanawake kutoka maeneo mbalimbali yakiwemo Wizara, mashirika na taasisi mbalimbali za umma na binafsi.

MATUKIO MBALIMBALI YA PICHA

DSC_0094Baadhi ya wanawake wa Chuo Kikuu Ardhi wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maandamano ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Temeke mwembe yanga. Continue reading WANAWAKE CHUO KIKUU ARDHI WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AHITIMISHA ZIARA ZA MIRADI MBALIMBALI KATIKA VIWANJA VYA CHUO KIKUU ARDHI

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AHITIMISHA ZIARA ZA MIRADI MBALIMBALI KATIKA VIWANJA VYA CHUO KIKUU ARDHI

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi jana alihitimisha ziara za kutembelea miradi mbalimbali inayofanywa na wilaya yake jana kwa kufanya mkutano katika viwanja vya Chuo Kikuu Ardhi, ambapo kabla ya kuanza mkutano Mhe. Hapi alifika ofisini kwa Makamu Mkuu wa Chuo kusaini kitabu cha wageni baadaye aliambatana na viongozi wa chuo kwaajili ya mkutano.

Mkutano huo ulikuwa kwaajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wake na kuruhusu maswali juu ya kero hizo. Aidha Mhe. Hapi aliambatana na wakuu wa idara mbalimbali wa wilaya ili kuweza kujibu kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Mhe. Hapi alimaliza kwa kuwashukuru wenyeji wake Chuo Kikuu Ardhi kwa kuwapatia uwanja wa kufanyia mkutano wa kuhitimisha ziara zake za kutembelea miradi mbalimbali katika wilaya yake.  

IMG-20170303-WA0008Mhe. Ally Hapi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni akiwa na viongozi wa Chuo Kikuu Ardhi kushoto ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Gabriel Kassenga, kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Mipango, Fedha na Utawala Prof. Evaristo Liwa. Continue reading MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AHITIMISHA ZIARA ZA MIRADI MBALIMBALI KATIKA VIWANJA VYA CHUO KIKUU ARDHI

Chuo Kikuu Ardhi chaeleza ushiriki wake katika masuala mbalimbali ya maendeleo ya uchumi na jamii nchini

Chuo Kikuu Ardhi chaeleza ushiriki wake katika masuala mbalimbali ya maendeleo ya uchumi na jamii nchini

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Idrissa Mshoro ameelezea ushiriki wa chuo chake katika baadhi ya masuala muhimu ya nchi na kutokana na taaluma zinazofundishwa na kufanyiwa tafiti na chuo chake.

Ameeleza hayo jana alipokuwa na mkutano na waandishi na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa habari maelezo, alisema utafiti huu unahusisha ujenzi wa kuta za jingo kwa kumimina mchanganyiko mahsusi wa saruji, mchanga na kemikali maalum kwa kutumia kingo za plastiki (plastic formwork) zinazoweza kutumika hadi mara hamsini baada ya matumizi ya awali. Continue reading Chuo Kikuu Ardhi chaeleza ushiriki wake katika masuala mbalimbali ya maendeleo ya uchumi na jamii nchini