KUFUNGULIWA RASMI KWA MFUMO WA ”AMIS” CHUO KIKUU ARDHI.

KUFUNGULIWA RASMI KWA MFUMO WA ”AMIS” CHUO KIKUU ARDHI.

Makamu Mkuu wa Chuo Prof.Evaristo J. Liwa amefungua rasmi mfumo wa ”AMIS” (Academic Management Information System) mnamo tarehe 7/03/2018 ni mfumo unaoratibu shughuli zote za kitaaluma hapa chuoni kwa mwaka 2017/18. Baadhi ya kazi zinazofanyika katika mfumo huu kwa sasa ni juu ya usajili, uwekaji wa matokeo, malazi na kuanza udahili kwa mwaka wa masomo 2018/2019. Pamoja na hayo pia mfumo huo utaendelezwa hapo baadaye kwa kuongeza kazi mbalimbali kama utaarishaji wa vitambulisho na ada za wanafunzi .

Mafunzo ya matumizi ya mfumo huo ulichukua muda wa siku mbili ambapo yalifanyika katika jengo la maktaba ya Chuo Kikuu Ardhi, wahusika walengwa walikuwa ni waandaaji na wasimamizi wa mitihani, Ofisi ya taaluma, Ofisi ya mshauri ya wanafunzi (DoS), wawakilishi wa usimamizi wa mitihani kutoka kila skuli.

Mfumo huu umetengenezwa chini ya kitengo cha Tehama (CICT) cha  Chuo Kikuu Ardhi.

IMG_0259

Prof.Evaristo Liwa akizindua rasmi AMIS kwa mara ya kwanza kabla ya mfumo huo kuanza kutumika Chuo Kikuu Ardhi.

IMG_0204

Dkt. Job Chaula aliyekuwa akiongoza timu nzima ya maandalizi ya matumizi ya AMIS akitoa maelezo juu ya mfumo huo kabla ya kuzinduliwa rasmi na Makamu Mkuu wa Chuo.

IMG_0278

Timu nzima iliyoaandaa mfumo huo wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo mara baada ya kuzindua mfumo huo rasmi.

IMG_0205

Washiriki wa mafunzo ya matumizi ya AMIS wakifuatilia maelekezo wakati wa mafunzo hayo.

IMG_0227

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo -Taaluma Prof. Gabriel Kassenga akitoa mchango wake siku ya kuhitimisha mafunzo hayo.

IMG_0217

Washiriki wakendelea kufuatilia mafunzo.

IMG_0157

Viongozi wa Chuo Kikuu Ardhi wakitazama namna mfumo utakavyokuwa unafanya kazi.

IMG_0198

Baadhi ya washiriki wakijadiliana

IMG_0207

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *