WANAWAKE WA CHUO KIKUU ARDHI KUSHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.
Wanawake wa Chuo Kikuu Ardhi wameshiriki maadhimisho ya siku wa wanawake duniani kwa kuungana na wenzao kutoka mashirika na vikundi mbalimbali vya wanawake wa Jiji la Dar es salaam mnamo tarehe 8/3/2018 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa mke wa Rais wa Jamuhuri wa Tanzania mama Janet Magufuli akiwa pamoja na mwenyeji wake mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe.Paul Makonda.
Meza ya mgeni rasmi pamoja na baadhi wa viongozi walioongozana katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani yalifanyika katika ukumbi wa mlimani city jijini Dar es salaam.
Wanawake wa Chuo Kikuu Ardhi wakiwa katika maandamano.
Chuo Kikuu Ardhi wanawake wakiwa nje ya ukumbi wa Mlimani City kabla ya kuanza rasmi.
Katika maandamano wakati wa kuingi ukumbini
Baadhi ya wanawake wa Chuo Kikuu Ardhi kabla ya kuanza maandamano.
Baadhi ya washiriki katika maadhimisho hayo ndani ya ukumbi wa Mlimani City.