MATUKIO YA PICHA MBALIMBALI MARA BAADA YA KAIMU NAIBU MAKAMU MKUU WA CHUO MIPANGO FEDHA NA UTAWALA PROF. ROBERT KIUNSI ALIPOTEMBELEA MTAMBO ULIOJENGWA KATIKA BANDARI YA TANGA NA CHUO KIKUU ARDHI AMBAPO UJENZI WA HATUA ZA AWALI UMEKAMILIKA 24-25 AGOSTI, 2016

MATUKIO YA PICHA MBALIMBALI MARA BAADA YA KAIMU NAIBU MAKAMU MKUU WA CHUO MIPANGO FEDHA NA UTAWALA PROF. ROBERT KIUNSI ALIPOTEMBELEA MTAMBO ULIOJENGWA KATIKA BANDARI YA TANGA NA CHUO KIKUU ARDHI AMBAPO UJENZI WA HATUA ZA AWALI UMEKAMILIKA 24-25 AGOSTI, 2016


img1

Timu ya wafanyakazi kutoka Chuo Kikuu Ardhi wakifanyamazungumzo na Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala Prof. Robert Kiunsi (alievaa shati la zambarau) mara baada yakuwasili jijini Tanga kwaajili ya kutembelea mradi wa Tide Gauge uliotengenezwa jijini hapo ambao umeshaanza kazi katika Bandari ya Tanga.

img2

Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Mipango, Fedha na Utawala Prof. Robert Kiunsi akisaini kitabu cha wageni  akifuatiwa na Mhandisi Hussein Rajab kutoka Chuo Kikuu Ardhi katika ofisi ya Kaimu meneja wa Bandari Tanga Bw. Tryphone Itambiko

img3

Prof. Robert Kiunsi pamoja na Mhandisi Hussein Rajabu kutoka Chuo Kikuu Ardhi mara baada ya kuwasili ofisini kwa Mhandisi Sapi Musa wa Bandari ya Tanga kabla ya kwenda sehemu ambako ndipo mtambo wa Tide Gauge ulipojengwa na Chuo Kikuu Ardhi.

img4

Prof. Robert Kiunsi alievaa shati la drafti akipata maelezo kutoka kwa Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu Ardhi Bw. Issa Hemed na timu yake  jinsi mashine ya Tide Gauge ambayo pichani haionekani inavyofanya kazi.

img5

Hivyo ndivyo mashine ya Tide Gauge inavyoonekana sambamba ni timu nzima kutoka Chuo Kikuu Ardhi mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa hatua ya kwanza ambapo sasa unaweza kufanya kazi.

img6

Mhadhiri mstaafu Issa Hemed wa Chuo Kikuu Ardhi akimuonyesha Prof. Robert Kiunsi pichani hayupo chumba cha mtambo wa Tide Gauge.

img7

Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala Prof. Robert Kiunsi wakiwa katika picha ya pamoja na timu nzima kutoka Chuo Kikuu Ardhi wa kwanzakulia ni Bw. Frank Gasper, Mhadhiri mstaafu Issa Hemed, Mhandisi Hussein Rajabu, upande wa kushoto wa kwanza ni Bw. Shafuri Mnzava na Bw. Pius Lugomela

img8

Hicho chombo kinatumika kupima kasi ya upepo, muelekeo wa upepo, joto la hewa, presha ya hewa na na hali ya hewa. ( Picha zote na Mary Kigosi-Chuo KIkuu Ardhi)

Leave a Reply

Your email address will not be published.