MAKAMU MKUU WA CHUO AKABIDHIWA VIKOMBE VYA USHINDI VYA MASHINDANO YA TUSA NA SHIMUTA

MAKAMU MKUU WA CHUO AKABIDHIWA VIKOMBE VYA USHINDI VYA MASHINDANO YA TUSA NA SHIMUTA

Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Evaristo Liwa amekabidhiwa vikombe vya ushindi vya TUSA upande wa wanafunzi na SHIMUTA kwa upande wa wafanyakazi. Zoezi hilo lilienda sambamba na kuwavalisha medani za ushindi na ugawaji wa vyeti kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi walioshiriki mashindano hayo.

DSC_0825Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi wakisikiliza taarifa fupi ya mashindano ya TUSA na SHIMUTA kutoka kwa Mwalimu wa michezo Bw. Boniface Tamba pichani hayupo.

DSC_0817Uongozi wa Chuo Kikuu Ardhi wakifuatilia taarifa fupi ya mashindano ya TUSA na SHIMUTA ilitolewa na Mwalimu wa michezo pichani hayupo. Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Evaristo Liwa, kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala Prof. Robert Kiunsi na kulia ni Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Prof. Livin Mosha.

DSC_0826Wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo Kikuu  Ardhi katika hafla fupi ya kukabidhi vikombe vya mashindano ya TUSA na SHIMUTA.

DSC_0837Mmoja wa wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi akikabidhi kikombe kwa Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Evaristo Liwa.

DSC_0843Mwakilishi wa wanafunzi akikabidhi kikombe cha ushindi kwa Makamu Mkuu wa Chuo.

DSC_0889Picha ya pamoja ya uongozi wa Chuo, serikali ya wanafunzi, wafanyakazi na wanafunzi mara baada ya kumaliza hafla ya kukabidhi vikombe vya ushindi wa mashindano ya TUSA na SHIMUTA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *