MAFUNZO YA UTENGENEZAJI WA BIOGAS NA MKAA JADIDIFU KUTOKANA NA TAKA, KWA WAKAZI WA MANISPAA YA BAGAMOYO
Chuo Kikuu Ardhi kupitia Shule ya Sayansi ya Mazingira na Teknolojia (SEST) imetoa mafunzo ya utengenezaji wa Biogas na Mkaa jadidifu kutokana na taka kwa wakazi wa Manispaa ya Bagamoyo. Mafunzo hayo yalitolewa Chuo Kikuu Ardhi katika jengo la Experimental tarehe 16 Januari, 2018.
Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Taaluma Prof. Charles Kihampa akitoa hotuba fupi siku ya ufunguzi wa mafunzo ya utengenezaji wa Biogas na Mkaa jadidifu kwa kutumia taka. Kulia kwake ni Dkt. Agnes Mwasumbi mwakilishi wa mradi wa SIDA -ARU ambao ndiyo wameandaa mafunzo hayo.
Washiriki kutoka Wilaya ya Bagamoyo wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya utengenezaji wa Biogas na Mkaa jadidifu kwa kutumia taka.
Bw. Jonas Gervas kutoka Chuo Kikuu Ardhi akitoa mada ya “Vyanzo vy taka na madhara yake katika mazingira na afya ya binadamu”
Bi. Minza Selele kutoka Chuo Kikuu Ardhi akiwaonesha washiriki jinsi ya kutengeneza Biogas kwa vitendo mara baada ya kuwasilisha mada ya “Uzalishaji wa Biogas kwa kutumia taka mbalimbali”
Bi. Minza Selele kutoka Chuo Kikuu Ardhi akiwasha jiko la gesi liliounganishwa na mtambo wa Biogas unaotengenezwa kwa kutumia taka mbalimbali.
Mmoja wa washiriki akiwasha jiko la gesi.
Dkt. Nyangi Chacha kutoka Chuo Kikuu Ardhi (mwenye miwani) akielezea jinsi wanavyozalisha mimea ambayo ni chakula cha mifugo kwa kutumia maji yanayojichuja katika mtambo wa kuzalishia Biogas.
Washiriki wakichanganya uji wa makaratasi na unga wa mbao tayari kwa maandalizi ya kuweka kwenye mashine na kutengeneza kuni.
Picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mafunzo hayo.