UONGOZI MPYA WA SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO KIKUU ARDHI WAAPA KIAPO CHA UAMINIFU

UONGOZI MPYA WA SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO KIKUU ARDHI WAAPA KIAPO CHA UAMINIFU

Mnamo tarehe 05/05/2017 katika ukumbi wa IHSS Serikali mpya ya wanafunzi ya chuo Kikuu Ardhi, walikula kiapo cha uaminifu katika kulinda na kutetea maslahi ya wanafunzi na Chuo kwa ujumla.

Hayo yalifanyika kufuatia kukamilika kwa uchaguzi ambapo Bw. Temba Gaspar aliibuka mshindi kwa nafasi ya Urais na Bw.  Maximilian James Makamu wa Rais wakati Waziri Mkuu ni Bw. Njau Godluck P.

Uongozi wa Chuo wakiwemo Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Idrissa Mshoro, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Prof. Gabriel Kassenga, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala Prof. Evaristo Liwa na Kaimu Mshauri wa Wanafunzi Bi. Amina Mdidi, walishuhudia viongozi mbalimbali wa serikali ya wanafunzi wakiwemo Rais, Makamu wa Rais, Spika, mawaziri wakiapa kutekeleza  majukumu yao ya kiuongozi kwa kufuata sheria na taratibu zote za Chuo.

DSC_0522Uongozi mpya wa serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu Ardhi (ARUSO) mbele kushoto ni Rais Bw. Temba Gaspar na Makamu wake Bw. Maximilian James.

20170505_171547Rais wa Serikali ya wanafunzi Bw. Temba Gaspar akiapa mbele ya Kaimu Jaji Mkuu Bw. Mbunda Antony H.

DSC_0538Kaimu Jaji Mkuu Bw. Mbunda Antony H. akisaini kiapo cha Makamu wa Rais Bw. Maximilian James pembeni yake.

20170505_181808Rais wa serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu Ardhi (ARUSO) Bw. Temba Gaspar akiongea mara baada ya kiapo.

20170505_175632Uongozi wa Chuo Kikuu Ardhi wa pili kutoka kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Idrissa Mshoro, wa kwanza ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Taaluma Prof. Gabriel Kassenga na kulia kwa Makamu Mkuu wa Chuo ni  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Mipango, Fedha na Utawala Prof. Evaristo Liwa na Kaimu Mshauri wa wanafunzi Bi. Amina Mdidi siku ya hafla fupi ya kuapishwa kwa uongozi mpya wa serikali ya wanafunzi (ARUSO).

DSC_0539Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Idrissa Mshoro akiongea na uongozi wa serikali ya wanafunzi siku ya hafla hiyo.

20170505_170359Baadhi ya viongozi wa serikali ya wanafunzi waliomaliza muda wao wakishudia tukio la kuapishwa kwa viongozi wapya kutoka kushoto ni Rais mstaafu Bw. Erasmus Kiwango na Makumu wake Bw. Christopher Christopher.

DSC_0549Picha ya pamoja mara baada ya kumaliza hafla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *