CHUO KIKUU ARDHI CHATEKELEZA AGIZO LA SERIKALI LA KUFANYA MAZOEZI YA VIUNGO KILA JUMAMOSI YA PILI YA MWEZI

CHUO KIKUU ARDHI CHATEKELEZA AGIZO LA SERIKALI LA KUFANYA MAZOEZI KILA JUMAMOSI YA PILI YA MWEZI

Katika kutekeleza agizo la serikali la kuwataka wananchi kufanya mazoezi ya viungo kila Jumamosi ya pili ya mwezi, uongozi wa Chuo Kikuu Ardhi ikishirikiana na Idara ya michezo iliandaa mazoezi ya viungo yaliyofanyika katika viwanja vya ARU ambapo yalitanguliwa na matembezi ya umbali wa kilomita tatu (3) yalioanzia jengo la Utawala la Chuo Kikuu Ardhi kuzunguka maeneo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mazoezi hayo yaliongozwa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Gabriel Kassenga sambamba na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo -Mipango, Fedha na Utawala Prof. Evaristo Liwa.

20170408_071825Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Gabriel Kassenga (katikati) kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo -Mipango, Fedha na Utawala Prof. Evaristo Liwa, kushoto ni Mkufunzi wa Michezo Bw. Boniface Tamba.

20170408_071921Baadhi ya wafanyakazi wa Chuo katika matembezi ya kilomita 3 kabla ya mazoezi ya viungo 

20170408_080838Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi wakifanya mazoezi ya viungo siku ya tarehe 08 Aprili, 2017 katika viwanja mara baada ya kumaliza matembezi ya kilomita 3

20170408_081227Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi wakifanya mazoezi ya viungo

20170408_081101

20170408_085451Wafanyakazi wakicheza mchezo wa kuvutana kamba siku hiyo ya Jumamosi

20170408_091502Picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mazoezi ya viungo siku ya Jumamosi 08 April, 2017

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *