KUFUNGWA KWA MTAMBO YA SATELLITE CHUO KIKUU ARDHI

KUFUNGWA KWA MTAMBO WA SATELLITE CHUO KIKUU ARDHI

Skuli ya Sayansi dunia, Uwekezaji katika miliki, Biashara na Infomatikia (SERBI) kwa udhamini wa   MESA (Monitoring for Environment and Security in Africa) wamefunga mtambo kwa ajili ya kunasa data za satellite (MODIS) na pia kutoa taarifa za majanga mbalimbali Kama Moto, mafuriko na ukame Kwa wakati nchini na maeneo ya SADC Kwa ujumla.

Katika kufanikisha hilo MESA walileta wataalaumu wawili ambao ni Bi. Masebo Rachel Nkepu kutoka Botswana na Bw. Mkise Steve Masha kutoka Afrika Kusini ili kuweza kutoa mafunzo mafupi kwa baadhi ya wataalamu kutoka Skuli ya Sayansi dunia, Uwekezaji katika Miliki, Biashara na Infomatikia juu ya uwezeshaji na ufuatiliaji wa mtambo huo ili kuweza kutunza kumbukumbu za majanga mbalimbali yanayoweza kutokea.

DSC_0064Bi. Masebo Rechal Nkepu kutoka Botswana akiweka lebo ya MESA mara baada ya kufungwa mtambo wa Satellite Chuo Kikuu Ardhi.

DSC_0073Mtambo wa Satellite uliofungwa ndani ya eneo la Chuo Kikuu Ardhi.

DSC_0067Wataalamu kutoka MESA na Chuo Kikuu Ardhi wakati wa kufunga mtambo wa Satellite.

DSC_0061

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *