CHUO KIKUU ARDHI CHAENDESHA MAFUNZO YA UONGOZI KWA VIONGOZI

CHUO KIKUU ARDHI CHAENDESHA MAFUNZO YA UONGOZI KWA VIONGOZI.

Chuo Kikuu Ardhi kimefanya mafunzo ya uongozi kwa viongozi wake katika idara mbalimbali Chuoni hapo yenye lengo la kuwakumbusha namna bora ya kuongoza na kuendesha vitengo wanavyovisimamia ili kuleta ufanisi na mahusiano mazuri mahali pa kazi.

Mafunzo hayo ya siku tatu yaliyoanza tarehe 12/11/2019 yanafanyika Chuoni hapo yakihudhuriwa na viongozi wakuu wa Chuo na viongozi wa idara mbalimbali Chuoni. Wawezeshaji ni wataalamu kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma, kampuni ya TSSL na Taasisi ya kitaifa ya uzalishaji (NIP)

Wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Evaristo Liwa aliwaasa viongozi kuwa mifano ya kuigwa kwa wale wanaowaongoza na pia kuzingatia misingi ya uongozi muda wote wanapokuwa wanatekeleza majukumu ya kitaasisi na ya vitengo vyao. Ameongeza kusema kuwa viongozi wanapaswa kuchukua hatua stahiki za kinidhamu kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma na kuepuka lugha za maudhi kwa watendaji walio chini yao.

Nae Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala Prof. Carolyne Nombo amewataka viongozi wanaohudhuria mafunzo hayo kuzingatia yote wanayoelezwa na wawezeshaji kwani azma ya Chuo na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuhakikisha wafanyakazi wote wanapata haki zao za msingi ikiwemo haki ya kusikilizwa na viongozi wao. Awali akimkaribisha Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Evaristo liwa kufungua mafunzo hayo Prof. Nombo alisema mafunzo yanayoendeshwa Chuoni yanaenda sambamba na sera ya utumishi wa umma inayozitaka taasisi kuwajengea uwezo wafanyakazi wake katika maswala mbalimbali ikiwemo maswala ya uongozi.

Akitoa ufafanuzi kuhusu mafunzo hayo, Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa Chuo Kikuu Ardhi Ndugu Essau Swila alisema ni vyema kwa viongozi wapya walioteuliwa kushika nyadhfa mbalimbali za uongozi chuoni kupatiwa mafunzo haya kwakuwa kiongozi anapaswa kuwa mfano bora kwa anaowaongoza .Aliongeza kusema kuwa, kiongozi katika utumishi wa serikali ni lazima kufahamu sheria, kanuni, nyaraka na miongozo mbalimbali ya serikali, kuzitunza na kuzifanyia kazi kwa mujibu na taratibu zilizowekwa.

20191113_093613

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Evaristo Liwa akiongea na washiriki wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uongozi Chuoni hapo.20191113_093544

Washiriki wa Mafunzo ya uongozi wakifuatilia kwa makini mafunzo yaliyokuwa yakiendeshwa.20191113_093043

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Mipango Fedha na Utawala Prof. Carolyne Nombo (wa kwanza kushoto) pamoja na Mkurugenzi Rasilimali watu na Utawala Ndugu. Essau Swilla (anaefuata) wakichukua maelezo muhimu wakati wa mafunzo hayo.20191113_092833

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala akisisitiza jambo kabla ya ufunguzi rasmi wa mafunzo ya uongozi.20191112_092449Muwezeshaji wa mafunzo kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Ndugu Charles Mgaya akiwasilisha mada.20191112_092151 (1)

Washiriki wa Mafunzo ya uongozi wakifuatilia mawasilisho kwa umakini Washiriki wakifuatilia mada mbalimbali