CHUO KIKUU ARDHI WATOA ELIMU MAADHISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

CHUO KIKUU ARDHI WATOA ELIMU MAADHISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

KATIKA kuadhimisha wiki ya utumishi wa Umma duniani Chuo Kikuu Ardhi (ARU) kimewatumia wataalam wake kutoa huduma za ushauri wa kitaalam katika maswala mbalimbali yanayohusu Ardhi na mazingira hususani upimaji ardhi na kupata hati miliki eneo la zahanati ya Goba jijini Dar es Salaam.
Pia wametoa huduma za usanifu majengo, ubunifu wa mandhari ya nje ya nyumba, uthamini wa mali, kujikinga na maafa kama vile mafuriko, uvunaji wa maji ya mvua na jinsi ya kuyahifadhi, huduma za mipango miji na upimaji ubora wa maji.
Washiriki wa maonesho hayo wamenufaika na huduma hiyo ya bure iliyotolewa kwa takribani siku mbili.

ARU TAT (1)

MHADHIRI wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) Paul Kitosi akifafanua jambo kwa sehemu ya wageni waliotembelea maonesho ya kazi zinazofanywa na chuo hicho wakati wa maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma Goba jijini Dar es Salaam leo. 

ARU MBI (1)

MHADHIRI wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Shule ya Sayansi ya Mazingira na Tekinolojia, Addo Michael Ndimbo akimwelezea mfumo wa usafishaji maji mmoja wa wageni waliotembelea maonesho ya chuo hicho katika maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma Goba jijini Dar es Salaam Juni 20 2019.

ARU MO (1)

MHADHIRI Msaidizi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) Dennis Gapser akitoa maelezo kwa sehemu ya wageni waliotembelea maonesho ya kazi zinazofanywa na chuo hicho wakati wa maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma Goba.

ARU NNE (1)MHADHIRI wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Dkt. Zakaria Ngereja akimwelimisha mkazi wa Dar es Salaam aliyekuwa na kiu ya kupata taarifa sahihi za maswala ya ardhi alipotembelea maonesho ya chuo hicho katika maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma Goba. 

ARU TANO (1)

MHADHIRI wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Dkt. Benedict Malele akifafanua jambo kwa baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam walioshiriki maonesho ya maswala ya ardhi yaliyoandaliwa na ARU eneo la Zahanati ya Goba katika maadhimisho ya wiki ya utumishi jijini humo.