JUMUIYA YA CHUO KIKUU ARDHI KUSHIRIKI BONANZA LA MICHEZO

JUMUIYA YA CHUO KIKUU ARDHI KUSHIRIKI BONANZA LA MICHEZO.

Chuo Kikuu Ardhi chini ya Idara ya Michezo kwa kushirikiana na uongozi wa Chuo Kikuu Ardhi waliandaa bonanza na michezo kwa wanajumuiya wa Chuo Kikuu Ardhi siku ya Tarehe 28. 6. 2019 katika viwanja vya Chuo Kikuu Ardhi.Bonanza hilo lilihusisha wafanyakazi na wanafunzo wote wa Chuo Kikuu Ardhi kwa kuandaa michezo na mbali mbali ikiwemo mazoezi ya viungo, kula apple, kukimbia,mpira wa miguu, mpira wa kikapu na kuvuta kamba.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo  Kikuu Ardhi Prof. Gabriel Kassenga alifungua rasmi zoezi hilo na kushiriki kuangalia baadhi ya michezo iliyoandaliwa na idara hiyo. Prof. G. Kassenga pia shiriki kuangalia mashindano ya michezo mbalimbali  ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi na kukabidhi zawadi kwa washindi wote walioshiriki na kuweza kutoka na ushindi katika michezo hiyo ikiwemo timu za wanafunzi na baadhi ya wafanyazi walioshiriki michezo hiyo.

Prof. Kassenga ambaye alikuwa ni ngeni rasmi katika bonanza hilo alipata nafasi ya kuzumza na wafanyakazi na wanafunzi walioshiriki zoezi hilo kwa kuwataka wawe wanajitokeza kwa wingi kwenye mazoezi na machizo mbalimbali inayoandaliwa na Chuo kwa lengo la kujenga mahusiano mahala pa kazi.IMG_6455

Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi walioshiriki Bonanza hilo wakiwa katika viwanja hivyo.

IMG_6586

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo -Taaluma Prof. Gabriel Kassenga (katikati) akiangalia michezo iliyokuwa inaendela katika viwanja vya Chuo Kikuu Ardhi. (kushoto) Bi. Amina Mdidi (kulia) ni Bi. Ann Mushi Kaimu Mkurugenzi Mkuu Rasilimali watu.

77d4a5e9-6290-4f25-b82a-a69853a41807(1)

Mkuu wa Bi. Amina Mdidi akifungua rasmi timu ya wanafunzi kwa upande wa mpira wa mguu

IMG_6499

Mkuu wa Idara ya Michezo Bw. Bonifance Tamba akiongoza mazoezi ya viungo kwa wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi.IMG_6537

wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi wakiendela kuangalia michezo iliyokuwa inaendelea uwanjani hapo.IMG_6589

Wanafunzi na Wafanyakazi walioshiriki mchezo wa kula Apple.IMG_6540

Washiriki waliojitokeza kwenye mashindano ya kukimbia.3aae6e93-5f1c-4ba3-bb7f-152973b20982

Mmoja wa mfanyakazi akipokea zawadi ya kuwa mshindi wa kwanza katika mchezo mashindano ya kukimbia

IMG_6573

Wanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi waliojitokeza kushiriki.bdb643e8-ccb2-4c85-8b3e-51e1541f7a12

IMG_64741de32164-4976-42e3-9195-11d4cf987e3b

Leave a Reply

Your email address will not be published.