MAFUNZO YA KUIMARISHA UADILIFU NA KUPAMBANA NA RUSHWA CHUO KIKUU ARDHI.
Chuo Kikuu Ardhi kupitia vitengo vyake mbalimbali kimefanya mafunzo ya kuimarisha na kupambana na rushwa na uimarishaji wa uelewa juu wa masuala ya kijinsia mahali pa kazi. Mafunzo hayo yamefanyika siku ya Ijumaa tarehe 28.6.2019 katika viwanja vya Chuo Kikuu Ardhi (Arch Plaza Ground) ambapo wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi walishiriki na kupata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali juu ya kupambana na rushwa na uelewa wa mambo ya kijinsia.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi -Taaluma Prof. Gabriel Kasenga alifungua mafunzo hayo kwa kuwataka washiriki watumie vizuri nafasi hiyo kwa kutoa ushirikiano kwa wawezeshaji walioandaliwa kutoa mada mbalimbali .Aliendelea kusema kuwa mafunzo hayo yatasaidia katika kuleta mchango chanya katika kuendesha shughuli mbalimbali katikamazingira ya kazi hapo Chuoni
Pamoja na mafunzo hayo yalioyokuwa yakiendelea katika viwanja hivyo vya Chuo Kikuu Ardhi, Zahanati ya Chuo Kikuu Ardhi pia iliendesha zoezi la upimaji wa afya kwa wafanyakazi wake ikiwemo upamaji wa Virusi vya Ukimwi na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama Kisukari, Presha (BP) kwa wafanyakazi wa Chuo.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma Prof. Gabriel Kassenga akifungua rasmi mafunzo hayo katika eneo la Chuo Kikuu Ardhi.(Kulia ni Bi. Anna Mushi Kaimu Mkurugenzi Mkuu Idara ya Rasilimali watu)
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Rasilimali watu Chuo Kikuu Ardhi Bi. Anna Mushi akizungumza machache na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi kabla ya mafunzo kuanza.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada zilizokuwa zikiendelea.
Bi. Marcella Salu kutoka TAKUKURU mkoa wa Kinondoni akitoa elimu juu ya kupambana na Rushwa kwa wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi.
Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi wakiendelea na Mafunzo.
Prof. Gabriel Kassenga akisalimia na baadhi wa wageni na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi.
Baadhi ya wafanyakazi waliojitokeza kupima afya zao wakati semina ikiwa inaendelea Chuo Kikuu Ardhi.
Baadhi yao wakipima uzito wa mwili na kupewa ushauri wa afya bora.
Mwentekiti wa kamati ya maadili Chuo Kikuu Ardhi Bw. Omary Kassim akiendesha utaratibu wa zoezi la mafunzo hayo Chuo Kikuu Ardhi.