CHUO KIKUU ARDHI CHAWANOA WAKUU WA IDARA, WATENDAJI NA WAJUMBE WA KAMATI YA MAAFA JIJINI DODOMA

CHUO KIKUU ARDHI CHAWANOA WAKUU WA IDARA, WATENDAJI NA WAJUMBE WA KAMATI YA MAAFA JIJINI DODOMA

Chuo Kikuu Ardhi kimetoa mafunzo ya uelewa wa maswala ya maafa kwa viongozi 27  katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wakiwemo wakuu wa Idara, Watendaji na Wajumbe wa Kamati ya Maafa.

Mafunzo hayo yalitolewa na Kitengo cha Mafunzo ya kukabiliana na Maafa cha Chuo Kikuu Ardhi yakilenga kuleta uelewa wa dhana ya maafa, mabadiliko ya tabia nchi na jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali katika ngazi ya Halmashauri ili kuyapunguza.

Mafunzo hayo yanaeleza pia jitihada mbalimbali zinazofanywa duniani kote katika kupambana na maafa na hatimaye kuyapunguza. Nchini Tanzania pamekuwepo na miundo mbalimbali ya kisera, kisheria, taratibu na miongozo kuhusu menejimenti ya maafa  pamoja na nini kifanyike ili kupunguza majanga na athari zake.

Kitengo cha Mafunzo ya kukabiliana na Maafa cha Chuo Kikuu Ardhi kimeshatoa mafunzo ya aina hii katika halmashauri nyingine za mkoa wa Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Tanga.

1

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Bi. Yustina W. Munishi akifungua Mafunzo ya uelewa wa maafa yaliyofanyika shule ya msingi Kaloleni.

IMG_7617Mkuu wa Kitengo cha Maafa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Robert Kiunsi akieleza kwa ufupi kuhusu mafunzo ya uelewa wa maafa.

IMG_7630Bw. Dionis Rugai akitoa mada ya uelewa kuhusu dhana ya maafa.

IMG_7656Dkt. Benedict Malele akiwasilisha mada ya miongozo na jitihada mbalimbali za kupambana na kupunguza maafa katika Dunia kwa washiriki ambao pichani hawapo.

IMG_7679

Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzo kutoka kwa Dkt. Benedict Malele pichani hayupo.

IMG_7667Bi. Catherine  Marimbo kutoka Idara ya Uratibu Maafa ofisi ya Waziri Mkuu akiwasilisha mada katika  mafunzo hayo.

IMG_7694

Leave a Reply

Your email address will not be published.