WAFANYAKAZI CHUO KIKUU ARDHI WAPEWA SOMO KUHUSU LUGHA ZA ALAMA

WAFANYAKAZI CHUO KIKUU ARDHI WAPEWA SOMO KUHUSU LUGHA ZA ALAMA

Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi wamepatiwa mafunzo elekezi kuhusu lugha za alama ili kuweza kurahisisha mawasiliano na jamii ya watu wenye dosari ya usikivu (Viziwi) Chuoni hapo. Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na wakufunzi kutoka Taasisi ya Maendeleo kwa  Viziwi Tanzania (TAMAVITA) yalijikita kwenye kutambua alama na ishara mbalimbali muhimu katika kuwasiliana.

Awali akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika Chuoni hapo Aprili 12, 2019 Mkurugenzi Rasilimali Watu ndugu Essau Swilla alisema, Chuo Kikuu Ardhi kinatekeleza Sera ya fursa sawa kwa wote hivyo Chuo kimeajiri baadhi ya wafanyakazi na kudahili  wanafunzi wenye changamoto mbalimbali za kimaumbile zikiwemo uziwi. Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa  adhma ya Chuo ni kuweka mazingira rafiki kwa watumishi na wanafunzi wenye changamoto mbalimbali ili nao wafurahie kuwa sehemu ya jumuiya ya Chuo.

Kwa upande wake Mkufunzi wa mafunzo hayo ndugu Karimu S. Bakari kutoka TAMAVITA amekipongeza Chuo Kikuu Ardhi kwa kutoa fursa za ajira na kupokea wanafunzi bila kujali changamoto mbalimbali walizokua nazo.

IMG-20190412-WA0102Mkurugenzi Rasilimali watu wa Chuo Kikuu Ardhi Bw. Essau Swilla akifuatilia mafunzo ya alama yaliyofanyika Chuoni hapo. 

IMG-20190412-WA0091Mkufunzi kutoka TAMAVITA Bw. Karimu S. Bakari akiwaelezea wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi matumizi ya lugha za alama katika mawasilino na viziwi.Kulia mwenye kiremba ni Mkalimani wa lugha za alama Bi.Maua Juma.

IMG-20190412-WA0096Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi wakionyesha lugha za vitendo wakati wa mafunzo. 

IMG-20190412-WA0094

Washiriki wa mafunzo ya lugha za alama wakiwa katika majaribio

IMG-20190412-WA0088

Washiriki wa mafunzo ya lugha za alama wakifuatilia mafunzo.IMG-20190412-WA0085Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya lugha za alama yaliyofanyika Chuo Kikuu Ardhi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *