WANAFUNZI BORA WA CHUO KIKUU ARDHI WAPEWA TUZO NA ZAWADI ZAO

WANAFUNZI BORA WA CHUO KIKUU ARDHI WAPEWA TUZO NA ZAWADI ZAO

Novemba 30 2018 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Profesa Evaristo Liwa alikabidhi zawadi kwa wanafunzi 98 waliofanya vyema katika masomo. Kati ya hao wasichana ni 51 sawa na asilimia 52 ya wanafunzi wote waliopata tuzo na wavulana ni  47 sawa na asilimia 48 ya wanafunzi wote ambao wamefuzu na kupata tuzo na zawadi mbalimbali kwa vipengele mbalimbali vya kitaaluma. Aidha Profesa Liwa amewapongeza wanafunzi wanaohitimu Desemba Mosi na wote waliojinyakulia zawadi mbalimbali kwa kuendeleza kuweka juhudi katika masomo kwa kipindi chote walichokuwa chuoni.

12Mwanafunzi Bora wa Jumla wa Chuo Kikuu Ardhi, Arnold Mushi akikabidhiwa vyeti na Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Evaristo Liwa wakati wa hafla ya kukabidhi wanafunzi 98 vyeti katika viwanja vya Chuo.

MARYMakamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Profesa Evaristo Liwa akimkabidhi cheti Mwanafunzi Bora Mary Chuwa wakati wa hafla ya kukabidhi wanafunzi 98 vyeti katika viwanja vya chuo hicho Dar es Salaam Novemba 30 2018.

ARU+LEOO

MSHINDI+WA+JUMLAMwanafunzi Bora wa Jumla wa chuo Kikuu Ardhi, Arnold Mushi akimkabidhiwa ua na mama yake mzazi, Fransisca Robert wakati wa hafla hiyo. Kulia ni mmoja pia wa wanafunzi Bora Mariamu Mohamed na mama yake (kushoto).

PAMOJA+NA+VCMakamu Mkuu wa chuo Kikuu Ardhi, Profesa Evaristo Liwa akiwa katika picha ya pamoja wanafunzi pamoja na wanataaluma wengine.

PAMOJAAMakamu Mkuu wa chuo Kikuu Ardhi, Profesa Evaristo Liwa akiwa katika picha ya pamoja na wanataaluma wengine. 

WAGENI

WASHIRIKI+TENA

WASHIRIKI

WASHIRIKII

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *