MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU ARDHI AZINDUA MAFUNZO YA VYUO VIKUU 12 VYA AFRIKA KUHUSU MBINU NA NAMNA YA KUTATHMINI ATHARI ZITOKANAZO NA MAAFA

MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU ARDHI AZINDUA MAFUNZO YA VYUO VIKUU 12 VYA AFRIKA KUHUSU MBINU NA NAMNA YA KUTATHMINI ATHARI ZITOKANAZO NA MAAFA

1T4A1202

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) Profesa Evaristo Liwa akiongea machache wakati wa ufunguzi wa kozi ya wiki mbili ya  kimataifa kuhusu maafa inayofanyika Chuo Kikuu Ardhi ikiwalenga wanafunzi wa shahada za juu na watendaji wa taasisi za kiserikali, binafsi na mashirika ya kimataifa. Washiriki wanatoka nchi 12 za Afrika na Mpango wa Chakula Duniani (WFP). Wakufunzi wa kozi wanatoka Vyuo Vikuu vya Afrika vinavyounda mwamvuli wa Periperi U, UNDP na WHO. Kozi  imefadhiliwa na UNDP, USAID/OFDA, WHO na WFP.  Kushoto ni Kaimu Naibu Mkuu Chuo Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Robert Kiunsi.

1T4A1204

Sehemu ya washiriki wa  kozi ya mafunzo ya mbinu za namna ya kutathmini athari zitokanazo na maafa wakifuatilia matukio wakati wa ufunguzi wa kozi hiyo  Septemba 10, 2018.

1T4A1191

Mkurugenzi wa Utafiti wa Majanga na  Mratibu wa Mradi wa Periperi U kutoka Chuo Kikuu cha Stellenbosch, Afrika Kusini Dk. Ailsa Holloway akiongea wakati wa ufunguzi wa  kozi hiyo. 

1T4A1215

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (Taaluma), Profesa Gabriel Kassenga (katikati) akibadilishana mawazo na Makamu Mkuu wa ARU, Profesa Evaristo Liwa (kulia) baada ya ufunguzi wa kozi hiyo Septemba 10, 2018. Kushoto ni Kaimu Naibu Mkuu Chuo Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Robert Kiunsi.

1T4A1178

1T4A1181

Sehemu ya washiriki wa  kozi ya mafunzo ya mbinu za namna ya kutathmini athari zitokanazo na maafa wakifuatilia matukio wakati wa ufunguzi wa kozi.

1T4A1228Sehemu ya wanahabari wakifanya mahojiano na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) Profesa Evaristo Liwa. Kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (Taaluma), Profesa Gabriel Kassenga.

1T4A1224

Mgeni rasmi Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) Profesa Evaristo Liwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kozi ya mafunzo ya mbinu za namna ya kutathmini athari zitokanazo na maafa .

Leave a Reply

Your email address will not be published.