NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA AFANYA ZIARA CHUO KIKUU ARDHI

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA AFANYA ZIARA CHUO KIKUU ARDHI.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe ametembela Chuo Kikuu Ardhi siku ya Ijumaa tarehe 6 Julai 2018. Katika ziara yake, Naibu Katibu Mkuu   amezungumza na uongozi wa Chuo Kikuu Ardhi juu ya masuala mbalimbali ya uendeshaji wa Chuo. Pia alipata fursa ya kuelezwa na kuona mipango mbalimbali mahsusi ya kimaendeleo ya Chuo.

Baada ya mazungumzo hayo alipata muda wakutembelea baadhi ya miradi ya ujenzi inayoendelea  Chuoni, maabara, na  tafiti . Naibu Katibu Mkuu aliambatana na baadhi ya viongozi wakiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Evaristo Liwa katika kutembelea sehemu hizo.

 

1

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.James Mdoe akiwa ofisini kwa Makamu Mkuu wa Chuo.

2

Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Evaristo Liwa akiwa na Naibu Katibu Mkuu ofisini kwake mara alipowasili Chuoni hapo.

4

Prof. Evaristo Liwa akizungumza kabla ya mkutano kuanza.

6

Mmoja ya waliohudhuria mkutano huo akijatambulisha katika mkutano.

5

Prof. James Mdoe akizungumza  wakati mkutano huo.

7

Baadhi ya wakuu wa vitengo  wakisikiliza kwa umakini.

8

Washirki wakifutilia mazungumzo.IMG_1436

Katika ni Rais wa serikali ya wanafunzi akizungumza katika mkutano huo.

9

Prof, Evaristo Liwa akiwa na ugeni wakielekea katika moja ya Jengo linaloendelea na ujenzi.

10

Prof. James Mdoe akiandika jina lake katika kitabu cha wageni mara alipofika katika eneo la ujenzi lililopo ndani ya Chuo Kikuu Ardhi linalojulikana kwa jina la “Lands building“.

11

Mhandisi Msimamizi wa Jengo hilo akitoa maelezo ya hatua wa ujenzi wa jengo hilo.

12

Dkt. Stalin Mkumbo akitoa maelezo kwa ugeni huo alipotembelea moja ya maabara .

13

Mmoja ya kifaa katika maabara hiyo.

15

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Ardhi akitoa maelzo mafupi juu ya mtambo wa kuchakata maji machafu (waste water treatment) uliotengenezwa na wataalamu wa Chuo.

16

Wakitazama mtambo huo kwa pamoja.

14

Bw. Ndimbo akionyesha baadhi ya vifaa katika maabara.

17

Picha ya pamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *