CHUO KIKUU ARDHI CHATOA ELIMU JUU YA KUPANGA KUSTAAFU

CHUO KIKUU ARDHI CHATOA ELIMU JUU YA KUPANGA KUSTAAFU

Chuo Kikuu Ardhi kwa kushirikiana na Shirika la Tija la Taifa imetoa elimu juu ya kupanga kustaafu kwa baadhi ya wafanyakazi wake wanaokaribia kustaafu ili waweze kupanga mpango wa kustaafu.

Mtoa mada Bw. Novatus Msemwa kutoka Shirika la Tija la Taifa alifundisha mada mbalimbali na mbinu wanazotakiwa kutumia mara baada ya kustaafu, baadhi ya mada alizofundisha ni kama zifuatazo jinsi ya kupanga kustaafu, kufikiria kustaafu, maisha baada ya kazi, masoko na huduma bora kwa wateja na usimamizi wa fedha.

Mafunzo hayo yametolewa Chuo Kikuu Ardhi siku ya Alhamisi tarehe 15/06/2018.

IMG_0881Bw. Novatus Msemwa kutoka Shirika la Tija la Taifa akitoa elimu kwa baadhi ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi ambao wanakaribia kustaafu pichani hawapo.

IMG_0906Uongozi wa Chuo Kikuu Ardhi wakifuatilia mafunzo ya kujindaa na kustaafu kutoka kwa mtoa wa mada pichani hayupo.

IMG_0898Baadhi ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi wakifuatilia mafunzo ya jinsi ya kujiandaa na kustaafu.

IMG_0903

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *