CHUO KIKUU ARDHI KUSHIRIKI MAONYESHO YA NISHATI WA MKAA KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAZINGIRA DUNIANI

CHUO KIKUU ARDHI KIMESHIRIKI MAONYESHO YA NISHATI WA MKAA KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAZINGIRA DUNIANI.

Chuo Kikuu Ardhi chini ya Skuli ya Sayansi ya Mazingira (SEST) kimeshiriki maonyesho ya nishati ya mkaa katika wiki ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani 31 Mei-5 Juni 2018 katika viwanja vya mnazi mmoja Dar es salaam, Maonyesho hayo yameshirikisha wadau mbalimbali kutoka  taasisi za serikali,zisizo za serikali,sekta binafsi,taasisi za utafiti,na vyuo vikuu kuonyesha bidhaa,ubunifu na uvumbuzi wao katika technolojia mbalimbali  za nishati za kupikia ambazo ni mbadala wa makaa. Chuo Kikuu Ardhi kimepata nafasi ya kutoa elimu hiyo na kuonyesha baadhi ya tecknolojia hiyo kwa kushirikisha walimu,wanafunzi na baadhi ya wanafunzi waliomaliza katika skuli hiyo.

1

Dkt. Chacha Nyangi Mkuu wa Idara ya Sayansi na Mazingira ya Chuo Kikuu Ardhi akiwa katika banda la maonyesho akieleza juu ya nishati jadidifu ya matumizi ya mkaa uliotengenezwa kwa kutumia taka asili za mimea.

5

Picha ya mkaa jadidifu zilitengenezwa na wataalamu wa Chuo Kikuu Ardhi  kwa kutumia taka asili za mimea.

a

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma Prof. Gabriel Kassenga alipotembelea banda la Chuo katika maonyesho hayo.

10

Baadhi ya wageni waliotembelea banda la Chuo katika viwanja vya maonyesho mnazi mmoja.

14

Moja ya mashine inayotumika kutengeneza mkaa jadidifuu wenye matobo madogo madogo.

8

Mr. Jonas Gervas kutoka Skuli ya Sayansi ya Mazingira ya Chuo Kikuu Ardhi akionyesha jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi.

4

12

13

11

7

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *