UONGOZI MPYA WA SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO KIKUU ARDHI WAAPA KIAPO CHA UAMINIFU

UONGOZI MPYA WA SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO KIKUU ARDHI WAAPA KIAPO CHA UAMINIFU

Mnamo tarehe 05/05/2017 katika ukumbi wa IHSS Serikali mpya ya wanafunzi ya chuo Kikuu Ardhi, walikula kiapo cha uaminifu katika kulinda na kutetea maslahi ya wanafunzi na Chuo kwa ujumla.

Hayo yalifanyika kufuatia kukamilika kwa uchaguzi ambapo Bw. Temba Gaspar aliibuka mshindi kwa nafasi ya Urais na Bw.  Maximilian James Makamu wa Rais wakati Waziri Mkuu ni Bw. Njau Godluck P.

Uongozi wa Chuo wakiwemo Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Idrissa Mshoro, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Prof. Gabriel Kassenga, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala Prof. Evaristo Liwa na Kaimu Mshauri wa Wanafunzi Bi. Amina Mdidi, walishuhudia viongozi mbalimbali wa serikali ya wanafunzi wakiwemo Rais, Makamu wa Rais, Spika, mawaziri wakiapa kutekeleza  majukumu yao ya kiuongozi kwa kufuata sheria na taratibu zote za Chuo.

DSC_0522Uongozi mpya wa serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu Ardhi (ARUSO) mbele kushoto ni Rais Bw. Temba Gaspar na Makamu wake Bw. Maximilian James. Continue reading UONGOZI MPYA WA SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO KIKUU ARDHI WAAPA KIAPO CHA UAMINIFU