MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AHITIMISHA ZIARA ZA MIRADI MBALIMBALI KATIKA VIWANJA VYA CHUO KIKUU ARDHI

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AHITIMISHA ZIARA ZA MIRADI MBALIMBALI KATIKA VIWANJA VYA CHUO KIKUU ARDHI

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi jana alihitimisha ziara za kutembelea miradi mbalimbali inayofanywa na wilaya yake jana kwa kufanya mkutano katika viwanja vya Chuo Kikuu Ardhi, ambapo kabla ya kuanza mkutano Mhe. Hapi alifika ofisini kwa Makamu Mkuu wa Chuo kusaini kitabu cha wageni baadaye aliambatana na viongozi wa chuo kwaajili ya mkutano.

Mkutano huo ulikuwa kwaajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wake na kuruhusu maswali juu ya kero hizo. Aidha Mhe. Hapi aliambatana na wakuu wa idara mbalimbali wa wilaya ili kuweza kujibu kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Mhe. Hapi alimaliza kwa kuwashukuru wenyeji wake Chuo Kikuu Ardhi kwa kuwapatia uwanja wa kufanyia mkutano wa kuhitimisha ziara zake za kutembelea miradi mbalimbali katika wilaya yake.  

IMG-20170303-WA0008Mhe. Ally Hapi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni akiwa na viongozi wa Chuo Kikuu Ardhi kushoto ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Gabriel Kassenga, kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Mipango, Fedha na Utawala Prof. Evaristo Liwa. Continue reading MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AHITIMISHA ZIARA ZA MIRADI MBALIMBALI KATIKA VIWANJA VYA CHUO KIKUU ARDHI