UFUNGUZI WA MAABARA YA KISASA CHUO KIKUU ARDHI
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi- Taaluma Prof. Gabriel Kassenga akiambatana na mgeni wake Mrs. Jasmien De Winne ambaye ni Mwakilishi wa ubalozi wa Belgium Tanzania, wamefungua rasmi maabara ya kisasa ya kufundisha Teknolojiya uendeshaji wa mitambo viwandani ,iliyopo Chuo Kikuu Ardhi.
Idara ya Mifumo ya Kompyuta na Hesabu iliyo chini ya Shule ya Sayansi za Dunia, Miliki, Biashara na Infomatikia (SERBI) iliyopo Chuo Kikuu Ardhi. Imepata ufadhili wa Maabara ya kisasa kwa lengo la kufundishia Teknolojia ya uendeshaji wa mitambo ya viwanda.Ufunguzi wa Maabara iyo ilifanyika Chuo kikuu Ardhi siku ya Ijumaa , tarehe 29, 2021.
Chuo kikuu Ardhi ni moja wa wafaidika kati ya vyuo sita kutoka nchi za Tanzania,Uganda na Ethiopia chini ya Mradi unaoitwa Applied Curricula in Technology for East Africa (ACTEA) ambapo baadhi ya washiriki katika mradi huo Chuo Kikuu Ardhi chini ya shule ya Sayansi za Dunia, Miliki, Biashara na Infomatikia (SERBI) wameweza kupata mafunzo ya siku tano kwa lengo la kuwajengea uwezo wa matumizi ya vifaa hivyo katika kufundisha.
Washiriki wa mafunzo hayo ni pamoja na wahadhiri kutoka vyuo vingine amabo nao ni wafaidika kutoka vyuo vingine ambao nao ni wafaidika ikiwemo Chuo Kikuu Mzumbe (Tanzania),Chuo Kikuu Muni, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbarara (Uganda) na Chuo Kikuu Jimma (Ethiopia).Mafunzo hayo yametolewa na wakufunzi kutoka Chuo cha Applied Sciences and Arts ( Ubeligiji)

Mrs. Jasmien De Winne Muwakilishi Ubalozi wa Ubeligiji akifungua rasmi maktaba hiyo
Continue reading UFUNGUZI WA MAABARA YA KISASA CHUO KIKUU ARDHI →